Alama za uakifishaji
Alama za uakifishaji hutumiwa katika uandishi ili kuiweka bayana sentensi, neno au kazi nzima husika. Ili kuafikia mawasiliano mwafaka, ni muhimu kutumia alama za uakifishaji kwa njia sahihi. Baadhi ya alama za uakifishaji ni kama zifuatazo:
Na
|
Alama
|
Jina la alama
|
Matumizi
|
Mfano
|
---|---|---|---|---|
1.
|
.
|
Nukta/kituo
|
Hutumiwa mwishoni mwatungo au sentensi.
|
Waliokuja jana wasogee mbele.
|
Hutumika katika uandishi wa vifupisho.
|
Dkt. = Daktari, n.k. = na kadhalika, k.v. = kama vile, prof. = profesa
| |||
Hutumika katika uandishi wa tarehe na namba zadesimali.
|
3.4.2015,
3.42
| |||
Hutumika mwishoni mwa orodha ya vitu.
|
Wanachapisha vitabuvya hisabati, historia,kiswahili, sayansi najiografia.
| |||
2.
|
,
|
Koma/mkato
|
Hutumika kuonyeshapumziko dogo katikasentensi.
|
Alipofika tu akamwita mtoto,lakini hakuitika.
|
Hutumika kutenganisha vitu vilivyoorodheshwa.
|
Alinunua papai,machungwa, maembe, ndizi na mapera.
| |||
3.
|
:
|
Nuktapacha
|
Kuunganisha vishazi huru viwili.
|
Watoto wanacheza:wakubwa wanafanya kazi
|
Kutenganisha dakika na sekunde.
|
Tuliwasili saa 2.30:29.
| |||
Kuonyesha vituvinavyotajwa kuwa viko katika orodha.
|
Katika ziara yakeatatembelea nchizifuatazo: Kenya,Uganda, Tanzania,Somalia na Ethiopia.
| |||
Kutenganisha Mada kuu na ndogo.
|
Historia ya Lugha: Kukua na kuenea kwake.
| |||
Kutenganisha juzuu na kurasa au mlango na mstari katika vitabu
|
Juzuu la 1: 2
Math. 5: 3-7
| |||
4.
|
!
|
Alama yakushangaa/mshangao
|
Baada ya maelezo ya kushangaza, kusisitiza, kushitua, kubeza au wito
|
Jamani! Amekufa.
Alidondoka puu!
Amina! Abee!
|
5.
|
?
|
Alama ya kuuliza
|
Hutumika katika maneno au tungo zinazoulizamaswali.
|
Kwa nini gharama yaumeme imepanda?
|
Kuonyesha neno autungo ya kushangaza nahuku ikiwa ni swali.
|
Hivi jana ulikutwa ofisini usiku?
| |||
6.
|
;
|
Nuktamkato
|
Kuunganisha dhana mbili katika sentesi ambatano.
|
Mshahara wa dhambi ni mauti; karama ya Mungu ni uzima wa milele.
|
Hutumika kabla ya kutaja maneno ambayo niviunganishi tegemezi.
|
Walipewa huduma zote muhimu; hata hivyo, waliamua kutoroka.
| |||
Hutumika kutenganisha vitu vilivyopo katikaorodha
|
Mkitaka kupita Kiswahili someni; kamusi, vitbu vyamashairi, riwaya
| |||
7.
|
( )
|
Parandesi
|
Hutumika kufungiamaelezo ya ziada katika tungo.
|
Matunda yote (maembe, ndizi na papai) yaliletwamezani.
|
Kuonyesha maelezo au mawazo ya mwandishiasiyekuwa mhusikakatika mchezo wakuigiza.
|
Alisafiri siku nyingi(takribani 25) jangwani
| |||
Kutenganisha namba au herufi zinazoorodheshavitu kwa idadi.
|
(1), (2), (3), (4)
(a), (b), (ch), (d)
| |||
8.
|
“ ”
|
Alama zaKunukuu (nukuu za alama moja)
|
Hutumika kuonyesha usemi ulionukuliwa
|
Baada ya mgomo, walimu walisema "Tutarejea darasani.”
|
Kutaja majina rasmi au yasiyo rasmi katika tungo.
|
Alipoingia “kigogo” tuwote walisimama.
| |||
‘ ’
| ||||
9.
|
…
|
Nukta katishi/alama zadukuduku
|
Huonyesha katikasentensi iliyoandikwa kuna baadhi ya manenoyamekatishwa.
|
Samaki mkunje, …
Ukiona vyaelea, …
|
Huonyesha maelezoyanayotolewa yanavutwa
|
Kwenye mstari …, kaatayari…,
Nenda… .
| |||
HUtumiwa kuonyesha sentensi isiyokamilika
|
Kama hizi ndizo siasa za kisasa, mimi...
| |||
10.
|
–
|
Alama ya kistari
|
Hutumika kuongezamaelezo ya ziada katika sentensi.
|
Mwalimu wetu – wahisabati- alitufundisha vizuri sana
|
Hutumika badala yanuktapacha kuonyeshamahojiano
|
Mzazi- Ulirejea saangapi?
Mtoto – Saa moja jioni.
| |||
Hutumika pamoja na alama za nukta pacha kuonyesha vitu vilivyoko katika orodha.
|
Walichangia vitu vingi: mavazi, vyakula, dawa na fedha
| |||
11.
|
’
|
Ritifaa
|
Huonyesha utamkaji wa nazali au ving’ong’o
|
Ng’arisha, ng’ata, ng’oa, ng’atuka
|
Huonyesha sehemuya neno au nambailiyoachwa kwa ajili ya kufupisha
|
’80 = 1980
U’shakula = umeshakula
| |||
12.
|
*
|
Kinyota
|
Huonyesha kuwa neno au sehemu ya maandishiiliyowekewa kinyota ina maelezo zaidi.
|
Tasfida* ilitumika sana kwa sababu kulikuwa na watoto.
*tasfida ni maelezoau maneno ya stahayasiyokuwa na matusi au ukosefu wa adabu.
|
Hutumika kamanuktakatishi kwakuonyesha kuwamaneno yanayokatishwayanahitaji tasfida.
|
Waliendekea namazungumzo, maramlango ukafungwa *** Sauti za kutisha.
| |||
13.
|
{ }
|
Mabanomawimbi/mabanodabali
|
Kubainisha orodha ya vitu vyenye sifa au vya kundi moja
|
Seti ya namba zakuhesabia: {0, 1, 2, 3, 4, 5...9}
|
14.
|
[ ]
|
Mabano mraba
|
Kubainisha maelezoya nyongeza ya matini chanzi
|
Alitumia msumenomashine [powersaw]kuvunja mlango
|
15.
|
( )
|
Parandesi
|
i) Kubainisha miundotegemezi katika tungo.
ii) Kubainisha orodha ya vipengele katika sentensi.
|
Mgeni (aliyekuja jana) ameondoka.
Nenda kalime haraka
|
16.
|
/
|
Mtoi
|
i) Alama hii inatumikabadala ya neno "au"
|
wanawake/wanaume
|
ii) Kutenganisha vitu viwili vyenye kazimoja
|
kit.ele/sic. = kitenzielekezi
| |||
iii) Husimama badala ya neno 'kwa'.
|
km 80/saa = kilometa sitini kwa saa moja
| |||
iv) Kubainishamatamshi
|
/m'tai/
|
USANIFU WA MAANDISHI:
JibuFuta🎓Usanifu wa maandishi katika fasihi ni kitendo au mchakato wa kuchambua mbinu mbalimbali za kifani/kisanaa zilizotumiwa na msanii katika kuiumba kazi yake ya fasihi.
Katika fasihi, usanifu wa maandishi huhusisha matini za aina tatu:
1.Riwaya/monolojia/masimulizi.
2. Tamthiliya/dayalojia/majibizano.
3. Ushairi (mashairi na tenzi).
🎓Mbinu za kisanaa/kifani zinazochambuliwa katika usanifu wa maandishi ni pamoja na:
A. Muundo:
👉Muundo ni mpangilio au mtiririko wa visa na matukio katika kazi ya fasihi .
👊Ikiwa matini ni Tamthiliya au riwaya , muundo waweza kuwa wa;
*moja Kwa moja (msago).
*muundo rukia/rejeshi/kioo.
✊Ikiwa matini ni Shairi, muundo hubainishwa Kwa kuangalia idadi ya mishororo(Mistari) katika beti zinazounda shairi hilo.
Miundo katika shairi ni kama ifuatavyo:
#Tamolitha/Monolitha- muundo wa shairi ambapo ubeti hujengwa na msitari mmoja tu.
#Tathnia- Mistari miwili katika ubeti
#Tathlitha- Mistari mitatu katika ubeti
#,Tarbia- Mistari minne katika ubeti
#Takhmisa- Mistari mitano katika ubeti
#Sabilia - Mistari sita na kuendelea katika ubeti.
B:Mtindo:
👉Ni namna au jinsi msanii anavyoiumba kazi yake ili kuipa upekee kati yake na wasanii wengine. Mtindo huhusisha Matumizi ya mbinu mbalimbali katika uandishi wa kazi za fasihi kama vile:
@Matumizi ya Taarifa ya habari.
@Matumizi ya matangazo.
@Matumizi ya mabango.
@Matumizi ya Nafsi
@ Matumizi ya Barua n.k
✊Ikiwa matini ni Shairi , mtindo hubainishwa Kwa kuangalia iwapo shairi linazingatia urari wa vina na mizani (mtindo wa kimapokeo) au iwapo shairi halijazingatia urari wa vina na mizani( Mtindo wa kisasa).
C . Matumizi ya Lugha .
👉 Usanifu wa maandishi huhusisha uchambuzi wa vipengele vikuu vitatu vya lugha, ambavyo ni:
#Tamathali za semi
#Semi mabalimbali.
#Mbinu nyingine za kisanaa.
-Vipengele hivi ndivyo huifanya lugha kuonekana nyepesi au ngumu katika matini hiyo.
D. Wahusika.
👉Katika katika za fasihi wahusika waweza kuainishwa Kwa vigezo vifuatavyo:
I: Kigezo cha Uhusika wa mhusika.
- Kwa kuzingatia kigezo hiki, kuna aina kuu mbili za wahusika:
(a). Wahusika wakuu
(b). Wahusika wadogo - Hawa wanaweza kuwa wasaidizi au wajenzi.
II: Kigezo cha Sifa /Tabia za mhusika.
- Kwa kuzingatia kigezo hiki ,kuna aina tatu za wahusika:
(a). Wahusika Duara
(b). Wahusika bapa
(c). Wahusika shinda/Foili.
✊Katika usanifu wa maandishi ni muhimu kubainisha wahusika na Uhusika wao katika matini husika.
E: Mandhari.
👉 Ni sehemu au mazingira ambamo matukio na matendo katika kazi ya fasihi hutendea au hutukia. Katika fasihi Mandhari yaweza kuwa halisi au ya kubuni.
- Ni muhimu kubainisha Mandhari katika matini husika .
🎓Mwl. Philemon Benard Masalu🎓

Nice sana sir but je unavyo vitabu ulivyoandika vya kiswahili??
JibuFutaNina swali,baadhi ya alama za uakifishaji Kuna waandishi husika au laa?
JibuFutaIvi
JibuFutaAhsante kwa maelezo mazuri
Iko sawa, kazi njema
JibuFutaMaswala yanayo ibuka kuhusiana na matumizi ya uakifishajl yako shwari kabisa shukran Kwa wadau wa kiswahili.
JibuFutaahsante kwa maelezo mazuri kwa haya makala. Yamekewa ya usaidizi mkubwa
JibuFutaKazi na maelezo mazuri.Ningependa kuwaagiza kuhusiana na utata unaotokana na utumiaji mbaya wa viakifishi
JibuFutaHaya makala yamenifaidi.Shukurani kwa Philemon .MwenyeziMungu akuzidishiye elimu na akupe afya uendele na kazi murwa.
JibuFutaKazi nzuri
JibuFutaNuktapacha, mkwaji,nukta za dukuduku,nuktamkato hutumika nini plz I need now ����
JibuFutaVipi kuhusu umuhimu wa kutumia alama za uandishi
JibuFutaNimeipenda matini Iko powa sana
JibuFutaKazi ipo vzuri mwl
JibuFuta