Jumapili, 14 Novemba 2021

KAULI ZA VITENZI VYA KISWAHILI

MADA KUU: MATUMIZI YA SARUFI MADA NDOGO: *KAULI ZA VITENZI VYA KISWAHILI* swali: Kauli ni nini? 👊*Kauli* ni - uhusiano uliopo baina ya kitenzi na kiima au kitenzi, kiima na shamirisho. au 👊*Kauli* -ni umbo la kitenzi linaloonesha uhusiano baina ya kiima na shamirisho. 👉Kauli za kiswahili huzalishwa na mnyambuliko wa vitenzi vya kiswahili ambao hupambanua: +tendo la mtu anayetenda/anayefanya +tendo la mtu anayetendwa/anayefanywa +tendo la mtu anayetendewa/anayefanyiwa +tendo liwezalo kutendeka/Kufanyika +tendo la mtu atendeshwaye/afanyishwaye n.k 👉Kauli za vitenzi vya kiswahili huwa na viambishi vijenzi (Vya mnyumbuliko) vyake maalumu kutokana na kanuni maalumu. *Kauli za kiswahili na ufafanuzi wake* ✍ *Kauli ya kutenda* 👉 Kauli hii hueleza tendo au Jambo ambalo mtendaji analitenda, amelitenda, alilitenda au atalitenda. 👉Katika Kauli hii kiima huwa na uamilifu wa kutenda. 👉Vitenzi vya Kauli hii huwa na *kiambishi tamati (alomofu ya Kauli) -"a*" baada ya mzizi hasa Kwa vitenzi vya asili ya kibantu. Mfano, Anachek-a, alisom-a, amelal-a n.k 👉Kwa vitenzi vyote visivyo na asili ya kibantu (aghalabu vya mkopo) mzizi wa kitenzi huwa katika Kauli ya kutenda pia mfano, anasali, atasamehe, atawaarifu, wameabudu, n.k ✍ *Kauli ya Kutendwa* 👉Ni Kauli ionyeshayo kiima au kitu au mtu fulani ni mwathirika au mpokeaji wa tendo fulani. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,e,i,o au u 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-W-"* mfano, pak-w-a, Chek-w-a, lim-w-a, som-w-a B: Ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na irabu a,i, au u 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Liw-"* mfano, Fagi-liw-a, chuku-liw-a, ti-liw-a C: Ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na irabu e na o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lew-"* mfano, tobo-lew-a, Bomo-lew-a, le-lew-a, poke -Lew-a. ✍ *Kauli ya Kutendea* 👉 Kauli hii huonesha kuwa mtendaji anatenda Kwa niaba, manufaa au faida ya mtu mwingine. 👉 Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,i na u 👉kiambishi cha Kutendea huwa *"-i-"* mfano, pig-i-a, pak-i-a, vunj-i-a. n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e na o 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-e-"* mfano, som-e-a, sem-e-a, omb-e-a n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na na umejengwa na irabu e na o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Le-"* mfano, to-le-a, tembe-le-a, bomo-le-a n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i, na u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-li-"* mfano, ti-li-a, vu-li-a, va-li-a n.k ✍ *Kauli ya Kutendewa* 👉Kauli hii huonesha kuwa kiima au mtu fulani ananufaika na tendo lifanywalo na mtu mwingine. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a, i,nau 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-iw-"* mfano, pak-iw-a, pik-iw-a, ruk-iw-a, n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e na o 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ew-"* mfano, som-ew-a, sem-ew-a, n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu e au o 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lew-"* mfano, zo -Lew-a, tembe-lew-a n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Liw-"* mfano, va-liw-a, ti-liw-a, vu-liw-a n.k ✍ *Kauli ya Kutendeka* 👉Kauli hii huonesha Hali ya Kutendeka au Kufanyika Kwa tendo fulani. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ik-"* mfano, pak-ik-a, pit-ik-a, ruk-ik-a, n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e au u 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ek-"* mfano, som-ek-a, chez-ek-a, n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu e au o 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-lek-"* mfano, zo-lek-a, tembe-lek-a, n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lik-"* mfano ti-lik-a, va-lik-a, vu-lik-a. n.k ✍ *Kauli ya Kutendana* 👉Kauli hii huonesha kuwa mtu fulani anamtenda mtu mwingine na mtu mwingine anamtenda mtu huyo. 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-an-"* mfano, pend-an-a, sem-an-a, vu-an-a, ti-an-a, zo-an-a, ruk-an-a, suk-an-a, pik-an-a n.k ✍ Kauli ya Kutendeana* 👉Kauli hii ni muunganiko wa Kauli mbili(kauli ya kutendea na kutendana). 👉Kauli hii huonesha kuwa mtu fulani anatenda Kwa niaba,faida au hasara ya mtu mwingine na Yule mwingine anatenda hivyo hivyo. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ian-"* mfano, pig-ian-a, pak-ian-a, ruk-ian-a n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e au o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ean-"* mfano, Chez-ean-a, som-ean- a, ot-ean-a, n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu e au o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lean-"* mfano, zo-lean-a, tembe-lean-a, to-lean-a, n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i,au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lian-"* mfano, va-lian-a, ti-lian-a, vu-lian-a. n.k ✍ *Kauli ya Kutendesha/Usababishi* 👉Kauli hii huonesha kuwa mtu fulani anasababisha kufanyika Kwa kitendo fulani Kwa mtu mwingine. 👉Kauli hii huwa na viambishi vijenzi vingi sana kama vile -ish-, -esh-, -lish- , -lesh-, -z-, -sh-, -iz-, -ez-, Liz, lez, -ny-, fy, vy, s. mfano, som-esh-a, chez-esh-a, imb-ish-a, va-lish-a, zo-lesh-a, to-lez-a, ko-lez-a, tok-ez-a, pend-ez-a, zoe-z-a, lege-z-a, chem-sh-a, ogo-fy-a, po-ny-a, Taka-s-a, To-s-a. n.k ✍ *Kauli ya Kutendua* 👉Kauli hii huonesha kuwa kinyume cha tendo fulani kimetendwa. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na irabu au konsonanti na umejengwa na irabu a,e,i,au u 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-U-"* mfano, Teg-u-a, pang-u-a, kunj-u-a fich-u-a,fung-U-a. B: Ikiwa mzizi unaishia na irabu au konsonanti na umejengwa na irabu O 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-O-"* mfano, Chom-o-a, n.k ✍ *Kauli ya Kutendata* 👉Kauli hii huonesha tendo la kufanya watu au vitu kushikana au kushikamanishwa. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-at-"* mfano, Fumb-at-a, kumb-at-a , pak-at-a, B: Ikiwa mzizi unaishia na irabu 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-t-"* mfano, oko-t-a, koko-t-a, n.k 👊 *Kauli Nyingine ni pamoja na*: ✍+ Kauli ya Kutenduka mf. Zib-uk-a ✍+ Kauli ya kutendama mf,Fich-am-a ✍+ Kauli ya kutendeshwa mf,som-esh-w-a, chez-esh-w-a. ✍+ Kauli ya Kutendeshea. mf, pig-ish-i-a, sem-esh-e-a, ✍+ Kauli ya kutendeshewa. mf, za-lish-iw-a, chez-esh-ew-a. ✍+ Kauli ya Kutendesheana. mf, pig-ish-ian-a, chez-esh-ean-a. ✍+ Kauli ya Kutendesheka. mf, Som-esh-ek-a, ig-iz-ik-a, chem-sh-ik-a. 👌 Kwa upande wa vitenzi vyote visivyo na asili ya kibantu Kanuni za utokeaji wa viambishi vijenzi Vya Kauli huwa hazizingatiwi sana . 💬Nukuu hizi zimeandaliwa na: 🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓 *MWL MASALU - IDARA YA KISWAHILI- SENGEREMA TRC OPEN SCHOOL - 14/11/ 2021* Mawasiliano: 👂philemonmasalu@gmail.com 👂0625506120/0689897806

Maoni 1 :