Jumatatu, 15 Novemba 2021
DHANA YA MZIZI WA NENO
*DHANA YA MZIZI Na SHINA LA NENO*
A: * MZIZI WA NENO*
Swali: Fafanua dhana ya MZIZI katika sarufi ya Kiswahili sanifu.
*MZIZI* 👉ni sehemu muhimu(kiini) zaidi ya neno ambayo haibadiliki badiliki na ambayo na ambayo hujenga maana ya msingi ya neno hilo.
au
*MZIZI* :👉 Ni sehemu ya neno ambayo ndiyo kiini cha maana na ambayo haiwezi kuchanganuliwa au kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza utambulisho wa neno hilo.
mfano, kaka, na, kisha, safi, wewe, Kwa n.k
*Mzizi wa kitenzi* : 👉Ni sehemu ya kitenzi ambapo maana ya kitenzi chenyewe hutokea/hujengeka.
au
*Mzizi wa kitenzi*: 👉 ni sehemu muhimu ya kitenzi isiyokuwa na viambishi vyovyote na ambayo haibadiliki badiliki.
👊Katika lugha ya Kiswahili sanifu, mzizi huweza kupokea viambishi awali au tamati, lakini mzizi hauwezi kugawanywa mara mbili(katika sehemu mbili) na kiambishi chochote.
mfano, A-ta-fik-ish-a, mzizi ni *-Fik-*
*AINA ZA MZIZI*
Swali: Dadavua aina za mzizi katika lugha ya Kiswahili.
👉Kuna aina kuu mbili (2) za mzizi katika lugha ya Kiswahili, ambazo ni:
✍ *Mzizi Huru*
👉Huu ni mzizi ambao unaweza kusimama peke yake kama neno lenye maana kamili pasi kuambikwa Kiambishi chochote.
👉Umbo la mzizi huru haliwezi kuvunjwavunjwa zaidi bila kuathiri ile maana yake ya msingi.
mfano, baba, hodari, dhaifu, Mimi,haraka, samehe, halafu, mbele, ya,na, tafiti, mama, dada,.
✊Baadhi ya mizizi huru huweza kupokea viambishi. hasa mizizi iliyotoholewa(isiyokuwa ya kibantu).
Mfano, sahau-lik-a, samehe-w-a,
✊Baadhi ya mizizi huru haiwezi kupokea viambishi vyovyote. Hii ni mizizi ya nomino za pekee (majina ya watu, wanyama n.k).
mfano, JUMATATU,, Juma, Simba, Yanga, Mwanza,n.k
✍ *Mzizi Funge*
👉Huu ni mzizi ambao hauwezi kujitegemea wenyewe kama neno lenye maana kamili pasi kufungamana na viambishi vingine.
Au
Ni mzizi ambao hauna kiambishi chochote na hivyo haujikamilishi kimuundo na kimaana kama neno kamili.
mfano, Chez-, lal-, imb-, Zo-, Va-, -O-, lim- n.k
Swali: unaelewa nini kuhusu dhana zifuatazo?
a. Mzizi asili.
b. Mzizi wa mnyumbuliko.
👏 *Mzizi asilia* : 👉ni mzizi wa kitenzi usio na kiambishi chochote.
mfano, Pik-, Som- Ig-
👏 *Mzizi wa mnyumbuliko*:👉 ni mzizi wa kitenzi ambao hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi vijenzi Vya Kauli(mnyumbuliko) pasi uwepo wa kiambishi tamati maana.
mfano, somesh-, vulian- Pikik-, chezesh- n.k
*Sifa za mzizi wa neno*
💣Ni mofu(umbo) muhimu zaidi kuliko mofu zingine zote katika neno kwani ndio huwa kiini kibebacho maana ya neno husika. Mzizi ukiondolewa katika neno, basi sehemu inayobaki huwa si neno tena.
💣Baadhi ya mizizi huweza kusimama peke yake bila viambishi kama maneno yenye maana kamili(hasa mizizi huru).
mfano, sahau, hivyo, lakini, n.k
💣Mizizi huwa haibadiliki badiliki wala kuvunjwavunjwa hata kama viambishi vitabadilika.
mfano, chez-ek-a, chez-esh-w-a, a-chez-a- ye
💣Maana ya msingi ibebwayo na mzizi huwa haibadiliki badiliki.
mfano, Lim- a, lim-ish-a, lim-ish-a, mzizi *-lim-* unabaki na dhana yake ya kuchimbua Ardhi.
💣Baadhi ya mizizi huweza kupokea viambishi na kuunda maneno mbalimbali ya mzizi huo.
mfano, Imb- a, imb-ik-a, Imb-ian-a, n.k
💣Baadhi ya mizizi huweza kuwekwa pamoja na kuunda mzizi changamano(ambatano).
mfano, -ana- + nchi = -ananchi.
-enye, + kiti = -enyekiti.
Nukuu hizi zimeandaliwa na
🎓 *MWL Philemon Benard MASALU*
*Idara ya Kiswahili -Sengerema TRC open school 2021*
mawasiliano: philemonmasalu@gmail.com.
0689897806/0625506120.
(15-11-2021)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Karibu sana kwa maoni yenye
JibuFutaSamahan je unaeza kuniambia kwa kutoa hoja nne kwa nn mzizi ni sehem ya msingi ya neno
FutaUmefafanua vyema sana nmekuelewa sana ebu andaa ufafanuzi mwngne dhana ya uambishaji na unyambulishaji
JibuFutaUnefafanua vizuri,naomba unifafanulie hatua za kupata mzizi wa neno.
JibuFutaAsanteni kwa maoni yenu nitafayafanyia kazi
JibuFutaTueleze pia dhana ya mofu ,alomofu na mofimu itatusaidia kaka
JibuFutaAsante kwa ufafanuz vp kuhusu utofauti wa shna na mzizi wa Nemo,
JibuFutaNaomba uandae uhusiano wa dhana ya mzizi,shina na kiini.
JibuFuta