Jumatatu, 15 Novemba 2021

DHANA YA MZIZI WA NENO

*DHANA YA MZIZI Na SHINA LA NENO* A: * MZIZI WA NENO* Swali: Fafanua dhana ya MZIZI katika sarufi ya Kiswahili sanifu. *MZIZI* 👉ni sehemu muhimu(kiini) zaidi ya neno ambayo haibadiliki badiliki na ambayo na ambayo hujenga maana ya msingi ya neno hilo. au *MZIZI* :👉 Ni sehemu ya neno ambayo ndiyo kiini cha maana na ambayo haiwezi kuchanganuliwa au kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza utambulisho wa neno hilo. mfano, kaka, na, kisha, safi, wewe, Kwa n.k *Mzizi wa kitenzi* : 👉Ni sehemu ya kitenzi ambapo maana ya kitenzi chenyewe hutokea/hujengeka. au *Mzizi wa kitenzi*: 👉 ni sehemu muhimu ya kitenzi isiyokuwa na viambishi vyovyote na ambayo haibadiliki badiliki. 👊Katika lugha ya Kiswahili sanifu, mzizi huweza kupokea viambishi awali au tamati, lakini mzizi hauwezi kugawanywa mara mbili(katika sehemu mbili) na kiambishi chochote. mfano, A-ta-fik-ish-a, mzizi ni *-Fik-* *AINA ZA MZIZI* Swali: Dadavua aina za mzizi katika lugha ya Kiswahili. 👉Kuna aina kuu mbili (2) za mzizi katika lugha ya Kiswahili, ambazo ni: ✍ *Mzizi Huru* 👉Huu ni mzizi ambao unaweza kusimama peke yake kama neno lenye maana kamili pasi kuambikwa Kiambishi chochote. 👉Umbo la mzizi huru haliwezi kuvunjwavunjwa zaidi bila kuathiri ile maana yake ya msingi. mfano, baba, hodari, dhaifu, Mimi,haraka, samehe, halafu, mbele, ya,na, tafiti, mama, dada,. ✊Baadhi ya mizizi huru huweza kupokea viambishi. hasa mizizi iliyotoholewa(isiyokuwa ya kibantu). Mfano, sahau-lik-a, samehe-w-a, ✊Baadhi ya mizizi huru haiwezi kupokea viambishi vyovyote. Hii ni mizizi ya nomino za pekee (majina ya watu, wanyama n.k). mfano, JUMATATU,, Juma, Simba, Yanga, Mwanza,n.k ✍ *Mzizi Funge* 👉Huu ni mzizi ambao hauwezi kujitegemea wenyewe kama neno lenye maana kamili pasi kufungamana na viambishi vingine. Au Ni mzizi ambao hauna kiambishi chochote na hivyo haujikamilishi kimuundo na kimaana kama neno kamili. mfano, Chez-, lal-, imb-, Zo-, Va-, -O-, lim- n.k Swali: unaelewa nini kuhusu dhana zifuatazo? a. Mzizi asili. b. Mzizi wa mnyumbuliko. 👏 *Mzizi asilia* : 👉ni mzizi wa kitenzi usio na kiambishi chochote. mfano, Pik-, Som- Ig- 👏 *Mzizi wa mnyumbuliko*:👉 ni mzizi wa kitenzi ambao hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi vijenzi Vya Kauli(mnyumbuliko) pasi uwepo wa kiambishi tamati maana. mfano, somesh-, vulian- Pikik-, chezesh- n.k *Sifa za mzizi wa neno* 💣Ni mofu(umbo) muhimu zaidi kuliko mofu zingine zote katika neno kwani ndio huwa kiini kibebacho maana ya neno husika. Mzizi ukiondolewa katika neno, basi sehemu inayobaki huwa si neno tena. 💣Baadhi ya mizizi huweza kusimama peke yake bila viambishi kama maneno yenye maana kamili(hasa mizizi huru). mfano, sahau, hivyo, lakini, n.k 💣Mizizi huwa haibadiliki badiliki wala kuvunjwavunjwa hata kama viambishi vitabadilika. mfano, chez-ek-a, chez-esh-w-a, a-chez-a- ye 💣Maana ya msingi ibebwayo na mzizi huwa haibadiliki badiliki. mfano, Lim- a, lim-ish-a, lim-ish-a, mzizi *-lim-* unabaki na dhana yake ya kuchimbua Ardhi. 💣Baadhi ya mizizi huweza kupokea viambishi na kuunda maneno mbalimbali ya mzizi huo. mfano, Imb- a, imb-ik-a, Imb-ian-a, n.k 💣Baadhi ya mizizi huweza kuwekwa pamoja na kuunda mzizi changamano(ambatano). mfano, -ana- + nchi = -ananchi. -enye, + kiti = -enyekiti. Nukuu hizi zimeandaliwa na 🎓 *MWL Philemon Benard MASALU* *Idara ya Kiswahili -Sengerema TRC open school 2021* mawasiliano: philemonmasalu@gmail.com. 0689897806/0625506120. (15-11-2021)

Jumapili, 14 Novemba 2021

KAULI ZA VITENZI VYA KISWAHILI

MADA KUU: MATUMIZI YA SARUFI MADA NDOGO: *KAULI ZA VITENZI VYA KISWAHILI* swali: Kauli ni nini? 👊*Kauli* ni - uhusiano uliopo baina ya kitenzi na kiima au kitenzi, kiima na shamirisho. au 👊*Kauli* -ni umbo la kitenzi linaloonesha uhusiano baina ya kiima na shamirisho. 👉Kauli za kiswahili huzalishwa na mnyambuliko wa vitenzi vya kiswahili ambao hupambanua: +tendo la mtu anayetenda/anayefanya +tendo la mtu anayetendwa/anayefanywa +tendo la mtu anayetendewa/anayefanyiwa +tendo liwezalo kutendeka/Kufanyika +tendo la mtu atendeshwaye/afanyishwaye n.k 👉Kauli za vitenzi vya kiswahili huwa na viambishi vijenzi (Vya mnyumbuliko) vyake maalumu kutokana na kanuni maalumu. *Kauli za kiswahili na ufafanuzi wake* ✍ *Kauli ya kutenda* 👉 Kauli hii hueleza tendo au Jambo ambalo mtendaji analitenda, amelitenda, alilitenda au atalitenda. 👉Katika Kauli hii kiima huwa na uamilifu wa kutenda. 👉Vitenzi vya Kauli hii huwa na *kiambishi tamati (alomofu ya Kauli) -"a*" baada ya mzizi hasa Kwa vitenzi vya asili ya kibantu. Mfano, Anachek-a, alisom-a, amelal-a n.k 👉Kwa vitenzi vyote visivyo na asili ya kibantu (aghalabu vya mkopo) mzizi wa kitenzi huwa katika Kauli ya kutenda pia mfano, anasali, atasamehe, atawaarifu, wameabudu, n.k ✍ *Kauli ya Kutendwa* 👉Ni Kauli ionyeshayo kiima au kitu au mtu fulani ni mwathirika au mpokeaji wa tendo fulani. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,e,i,o au u 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-W-"* mfano, pak-w-a, Chek-w-a, lim-w-a, som-w-a B: Ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na irabu a,i, au u 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Liw-"* mfano, Fagi-liw-a, chuku-liw-a, ti-liw-a C: Ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na irabu e na o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lew-"* mfano, tobo-lew-a, Bomo-lew-a, le-lew-a, poke -Lew-a. ✍ *Kauli ya Kutendea* 👉 Kauli hii huonesha kuwa mtendaji anatenda Kwa niaba, manufaa au faida ya mtu mwingine. 👉 Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,i na u 👉kiambishi cha Kutendea huwa *"-i-"* mfano, pig-i-a, pak-i-a, vunj-i-a. n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e na o 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-e-"* mfano, som-e-a, sem-e-a, omb-e-a n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na na umejengwa na irabu e na o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Le-"* mfano, to-le-a, tembe-le-a, bomo-le-a n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i, na u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-li-"* mfano, ti-li-a, vu-li-a, va-li-a n.k ✍ *Kauli ya Kutendewa* 👉Kauli hii huonesha kuwa kiima au mtu fulani ananufaika na tendo lifanywalo na mtu mwingine. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a, i,nau 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-iw-"* mfano, pak-iw-a, pik-iw-a, ruk-iw-a, n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e na o 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ew-"* mfano, som-ew-a, sem-ew-a, n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu e au o 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lew-"* mfano, zo -Lew-a, tembe-lew-a n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Liw-"* mfano, va-liw-a, ti-liw-a, vu-liw-a n.k ✍ *Kauli ya Kutendeka* 👉Kauli hii huonesha Hali ya Kutendeka au Kufanyika Kwa tendo fulani. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ik-"* mfano, pak-ik-a, pit-ik-a, ruk-ik-a, n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e au u 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ek-"* mfano, som-ek-a, chez-ek-a, n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu e au o 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-lek-"* mfano, zo-lek-a, tembe-lek-a, n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lik-"* mfano ti-lik-a, va-lik-a, vu-lik-a. n.k ✍ *Kauli ya Kutendana* 👉Kauli hii huonesha kuwa mtu fulani anamtenda mtu mwingine na mtu mwingine anamtenda mtu huyo. 👉Kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-an-"* mfano, pend-an-a, sem-an-a, vu-an-a, ti-an-a, zo-an-a, ruk-an-a, suk-an-a, pik-an-a n.k ✍ Kauli ya Kutendeana* 👉Kauli hii ni muunganiko wa Kauli mbili(kauli ya kutendea na kutendana). 👉Kauli hii huonesha kuwa mtu fulani anatenda Kwa niaba,faida au hasara ya mtu mwingine na Yule mwingine anatenda hivyo hivyo. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu a,i au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ian-"* mfano, pig-ian-a, pak-ian-a, ruk-ian-a n.k B: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti na umejengwa na irabu e au o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-ean-"* mfano, Chez-ean-a, som-ean- a, ot-ean-a, n.k C: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu e au o 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lean-"* mfano, zo-lean-a, tembe-lean-a, to-lean-a, n.k D: Ikiwa mzizi unaishia na irabu na umejengwa na irabu a,i,au u 👉 kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-Lian-"* mfano, va-lian-a, ti-lian-a, vu-lian-a. n.k ✍ *Kauli ya Kutendesha/Usababishi* 👉Kauli hii huonesha kuwa mtu fulani anasababisha kufanyika Kwa kitendo fulani Kwa mtu mwingine. 👉Kauli hii huwa na viambishi vijenzi vingi sana kama vile -ish-, -esh-, -lish- , -lesh-, -z-, -sh-, -iz-, -ez-, Liz, lez, -ny-, fy, vy, s. mfano, som-esh-a, chez-esh-a, imb-ish-a, va-lish-a, zo-lesh-a, to-lez-a, ko-lez-a, tok-ez-a, pend-ez-a, zoe-z-a, lege-z-a, chem-sh-a, ogo-fy-a, po-ny-a, Taka-s-a, To-s-a. n.k ✍ *Kauli ya Kutendua* 👉Kauli hii huonesha kuwa kinyume cha tendo fulani kimetendwa. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na irabu au konsonanti na umejengwa na irabu a,e,i,au u 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-U-"* mfano, Teg-u-a, pang-u-a, kunj-u-a fich-u-a,fung-U-a. B: Ikiwa mzizi unaishia na irabu au konsonanti na umejengwa na irabu O 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-O-"* mfano, Chom-o-a, n.k ✍ *Kauli ya Kutendata* 👉Kauli hii huonesha tendo la kufanya watu au vitu kushikana au kushikamanishwa. 👉Viambishi vijenzi Vya Kauli hii huwa kama ifuatavyo: A: Ikiwa mzizi unaishia na konsonanti 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-at-"* mfano, Fumb-at-a, kumb-at-a , pak-at-a, B: Ikiwa mzizi unaishia na irabu 👉kiambishi kijenzi cha Kauli hii huwa *"-t-"* mfano, oko-t-a, koko-t-a, n.k 👊 *Kauli Nyingine ni pamoja na*: ✍+ Kauli ya Kutenduka mf. Zib-uk-a ✍+ Kauli ya kutendama mf,Fich-am-a ✍+ Kauli ya kutendeshwa mf,som-esh-w-a, chez-esh-w-a. ✍+ Kauli ya Kutendeshea. mf, pig-ish-i-a, sem-esh-e-a, ✍+ Kauli ya kutendeshewa. mf, za-lish-iw-a, chez-esh-ew-a. ✍+ Kauli ya Kutendesheana. mf, pig-ish-ian-a, chez-esh-ean-a. ✍+ Kauli ya Kutendesheka. mf, Som-esh-ek-a, ig-iz-ik-a, chem-sh-ik-a. 👌 Kwa upande wa vitenzi vyote visivyo na asili ya kibantu Kanuni za utokeaji wa viambishi vijenzi Vya Kauli huwa hazizingatiwi sana . 💬Nukuu hizi zimeandaliwa na: 🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓 *MWL MASALU - IDARA YA KISWAHILI- SENGEREMA TRC OPEN SCHOOL - 14/11/ 2021* Mawasiliano: 👂philemonmasalu@gmail.com 👂0625506120/0689897806